MWANAMUZIKI FERGUSON WA BENDI YA MASHUJAA KUWASILI KESHO KUTOKA SAUZ


MWANAMUZIKI wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa, Saulo John ‘Ferguson’. aliyekuwa mapumzikoni nchini Afrika Kusini anarejea nchini kesho  na usiku ataanza kufanya vitu vyake kwenye ukumbi wa San Siro.

Akimzungumza Dar es Salaam leo meneja wa hiyo King Dodoo la Buche, alisema kuwa mwanamuziki huyo aliyekuwa mapumzikoni nchini humo anarejea na kuanza kazi yake kesho.

Alisema kuwa mwamuzi huo ambaye ameahidi kurudi na vitu vipya kutoka nchini huko.

Alisema katika onesho hilo Furguson atatumia nafasi hiyo kuwaonjesha vionjo vipya alivyotunga akiwa nchini humo.

Naye Furguson ambaye alizungumza na Gazeti hili juzi kwa njia ya simu akiwa nchini huko ‘Ferguson’ katika mapumziko hayo ameweza kupata mawazo ya kubuni rapu mpya ambazo zitaanza kutumika katika bndi yake hiyo.

Ferguson alisema amejipanga kuanza kuonesha rapu hizo wiki hiyo kuanzia katika onesho lake la kwanza ambalo litafanyika katika ukumbi wa SunSiro siku ya Alhamis.

Alisema kuwa katika ziara yake hiyo ya nchini Afrika Kusini ilikuwa na mafanikio makubwa licha ya kuwepo ukweni.

"Nilikuwa nimeenda ukweni kwangu...lakini nimepata vitu vipya ambavyo tutavifanya  na wanamuziki wenzangu wa Mashujaa na

kuleta mabadiliko makubwa katika bendi yetu"alisema Ferguson.

Alisema mara baada ya kusaini mkuataba wake alimua kwenda

kuona wakwe zake nchini  humu ambapo amekaa kwa muda wa siku 10.

Ferguson, alisema kwa kutambua mchango wa wanamuziki wenzake katika kuleta mabadiliko katika soko la muziki wa ndansi hapa nchini watakaa na kuangalia wafanye nini zaidi ili bendi yao iweze kuja kivingine.

Hivi karibuni bendi hiyo ilipata wanamuziki wapya, ambao ni Sudi Mohamed ‘MCD’, Charles Gabriel ‘Chalz baba’, Lilian Tungalaza Internet, na Ally Akida kutoka bendi ya Twanga Pepeta.

Mashujaa Ijumaa itakuwa na onesho lake katika ukumbi wa Business Park uliopo Kijonyama wakati Jumapili jioni itakuwa kwenye Bonanza la kila wiki kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA