NAIBU WAZIRI MAJI ATAKA WALIOPATA HATI MASHAKA WAWAJIBISHWE


Naibu Waziri wa Maji, Bilithin Mahenge akifungua  mkutano wa  mkuu wa  13 wa mwaka wa mamlaka hizo unaendelea kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza
 
 
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
 
 NAIBU Waziri wa Maji, Binilith Mahenge ameziagiza  bodi za Mamlaka ya Maji safi na  Majitaka mijini   kuwachukulia  watumishi wote  hatua  zinazostahili , ambao  wamesababisha mamlaka zilizopata hati zenye mashaka   katika  Taarifa ya  Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka hizo kwa mwaka fedha uliopita(2010/2011).
 Kauli hiyo imetolewa leo(jana) na Naibu Waziri huyo wakati alipofungua mkutano mkuu   wa 13  wa mamlaka hizo unaendelea kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku mbili umehusisha  watu 200 ambao ni  wakurugenzi, watalaamu wa  wizara hiyo, TAMISEMI, Wenyeviti wa Bodi na Watendaji  Wakuu wa  EWURA, DAWASA na DAWASCO  na wadau wengine.
Mada kuu ya mkutano huo ni “Kuzijengea Mamlaka  Uwezo wa Rasilimali watu katika Kutoa Huduma Endelevu”
“ Ukaguzi  wa Hesabu za Mamlaka na ripoti zake ni kioo muhimu cha kupima uttendaji kazi, usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwenye mamlaka… Sikuridhika na kiwango cha kuongezeka   mamlaka zilizopata hati zenye mashaka  kutoka tatu  mwaka 2009 /2010 hadi tano mwaka 2010/2011. Tegemeo langu mamlaka zote  zipate hati safi ya ukaguzi wa hesabu.  
 Naibu Waziri Mahenge  alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Mtwara, Musoma, Songea, DAWASA na DAWASCO, ambapo alizitaka kuongeza nguvu katika usimamizi wa fedha katika mamlaka zao kwa kuhakikisha hesabu za mamlaka hizo zinatayarishwa kwa usahihi  unaokubalika n kuondoa kasoro zilizojitokeza.
Aidha Mahenge aliongeza kuwa kasi ndogo ya utekelezaji wa program ya miradi ya maji  iliyopangwa inachangiwa na uhaba wa fedha kwa kiasi kikukubwa na upungufu wa wataalamu wanaoweza kusimamia kwa makini utekelezaji wake kuanzia ngazi za mikoa , wialya, miji midogo na miradi ya kitaifa.
Aliyataja maeneo yenye upungufu kuwa ni  usimamizi fedha za miradi, ununuzi, utoaji taarifa za utekelezaji wa miradi, ukusanyaji na utoji wa taarifa za miradi, uchambuaji na utunzaji takwimu.
Alisema hali hiyo inaonyesha umhimu wa kujenga uwezo kwa watendaji katika ngazi zote ili mapungufu yaliyopo yasiendelee kuonekana, hivyo alizitaka bodi hizo kuwa na mipango ya mafunzo inayotekelezeka na kulenga mapungufu hayo.
Mahenge alisema changamoto nyingine  katika utkelezaji wa program ya maendele ya sekta ya maji ni kuchelewa kwa fedha za maendeleo kutoka wadau wa maendeleo, hali ambyo imesababisha  wakandarasi kupunguza kasi ya ujenzi na kutoza riba, ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa ujenzi.
Alisema uchelewaji wa malipo unatokana na hasa na uchelewashaji wa taarifa za utekelezaji kutokakwa watekelezaji wa ngazi zote. Hivyo hadi kufikia Aprili mwaka huu jumla ya sh. bilioni 32.7 hajijalipwa kati ya hizo fedha za wakandarasi ni sh. bilioni 30.1 na wahandisi washauri ni sh. bilioni 2.6.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhadisi Christopher Sayi alisema  katika jiji la Dares Salaam na maeneo yanayohudumiwa na DAWASCO, kiwango cha utaoji wa huduma ya majisafi kimeshuka na kufikia asilimi 51kipindi cha mwezi Juni,2011 kutoka asilimia 55 ya Juni 2010.
Alisema upungufu huo umetokana na kupungua kwa uzalishajimaji uliosababishwa na  mgao wa umeme na ongezeko la maeneo ya utoaji huduma kwa kupanuka kwa jiji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA