Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba atembelea TCRA

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kushoto), wakati alipotembelea Makao Makuu ya ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania zilizopo jengo la Mawasiliano Tower Barabara ya Sam Najoma jijini Dar es Salaam jana kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akimsikiliza Mhandisi Mfawidhi wa Mawasiliano ya Redio wa Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania, Johannes Magesa wakati alipokuwa akitoa maelezo juu ya kutambua muingiliano wa mawasiliano kwa masafa ya redio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma.

Naibu Waziri Makamba (kulia) akimsikiliza Mhandisi wa TCRA, Ikuja Jumanne wakati m aliokuwa akionyeshwa kifaa cha kupimia Masafaa ya Redio na TV, wakati alipotembelea TCRA.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma wakionyeshwa kifaa kinachotumika kupimia mionzi ya minara mbalimbali hapa nchini na Meneja wa Mipango na Utafiti wa TCRA, Dk. Ali Simba.

Afisa Habari wa TCRA, Bi. Doris akiwa na wafanyakazi wenzake wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mheshimiwa Makamba alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI