Nchunga ajibu mashambulizi Yanga

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Lloyd Nchunga amesema anajua wa kumkamata endapo atadhurika kutokana na kauli mbalimbali zinazotolewa na wanachama kuhusu yeye.

Tangu kufungwa mabao 5-0 na Simba katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara, hali ndani ya Yanga imekuwa si shwari baada ya wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kumtaka Nchunga ang’oke katika klabu hiyo kwa madai kuwa kaifikisha pabaya.

Mbali na kufungwa idadi hiyo ya mabao na mtani wake wa jadi, Yanga pia ilishindwa kutetea ubingwa wake wa bara na pia ilitolewa mapema kwenye michuano ya Kimataifa ambapo ilikuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nchunga alisema anajua kila kitu kinachoendelea kutokana
na vurugu hizo na wanaoendesha mgogoro huo na kwamba hana wasiwasi kwani endapo atadhurika kwa namna yoyote anajua nani amkamate.

“Mimi ombi langu ni moja tu kwa wanachama, wasubiri mkutano mkuu wa klabu Julai 15 hapo ndipo watazungumza kila wanalotaka badala ya kuzungumzia vijiweni,” alisema. “Kuna watu wanapenda kukaa na kuzungumza vitu ambavyo havina ukweli, ninachoomba kikubwa ni watu wasikae kusikiliza maneno ya mtaani wasubiri mkutano mkuu na mimi nikidhurikanajua nani wa kumkamata maana kuna watu wanazungumza vitu tofauti na vilivyopo,” alisema.

Akifafanua kuhusu madai ya kwamba uongozi wake unadaiwa na wachezaji wote, Nchunga alisema anachofahamu kama mwenyekiti ni kwamba anadaiwa na wachezaji wawili ambao ni Nourdin Bakari na Jerryson Tegete.

“Hayo madai ya kwamba Sh milioni 150 ambazo Yusuf Manji (Aliyekuwa mfadhili wa Yanga)
alilipia ada ya kadi za wanachama kwa miaka miwili pamoja na Sh milioni 50 za uhamisho wa Mrisho Ngassa aliyekwenda Azam zilitumika katika usajili na si kama baadhi ya watu wanavyodai,” alifafanua Nchunga.

Nchunga alisema anashangaa madai ya kwamba uongozi wake umefuja Sh milioni 750: “Madai
hayo hayana ukweli wowote hivi vitu vya ajbu sana,” alisema Nchunga.

Tayari kamati ya Utendaji ya Yanga imeanza ‘kumeguka’ baada ya baadhi ya wajumbe wake kujiuzulu akiwemo aliyewahi kuwa mchezaji wake, Ali Mayay.

                     

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.