OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA YATEKELEZA AGIZO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KWA KUTENGA SIKU MAALUM YA USAFI WA MAZINGIRA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifyeka maua kuyaweka sawa katika moja ya bustani katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais inayozitaka taasisi za Umma na Serikali kuwa na siku maalum ya usafi wa mazingira katika maeneo yao. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa imejiwekea utaratibu wa kufanya usafi kila siku ya alhamisi ya wiki ambapo kila mtumishi anashiriki katika jukumu hilo. Usafi huo huanza saa mbili hadi saa tatu asubuhi. Miongoni mwa kazi zinazofanyika ni pamoja kufagia, kufyeka, uzoaji wa taka ngumu, na usafi wa jumla katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
 Zoezi la usafi likiwa linaendelea
Kutoka kushoto ni Afisa Elimu Taalum Mkoa Domician Chose na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Frank Jailos Mateny wakijumuika kwenye usafi huo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akipeana neno la mwisho na watumishi wake mara baada ya zoezi hilo la usafi kukamilika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI