RAIS OBAMA AUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA.

RAIS wa Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii kwa kutambua uhusiano huo.

Lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja.
Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa za jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani. 

Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za aina hii.
Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.
Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*