RASMI SIMBA BINGWA, AZAM WATOKOTA


Kikosi cha Simba kilichotwaa ubingwa leo kikiwa kambini Zanzibar, baada ya Mtibwa Sugar kuituliza Azam kwa kichapo cha mabao 2-0.

SIMBA leo wanaanza kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Azam FC kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ina pointi 59, ambazo sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote msimu huu na imebakiza mechi moja dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili ambayo kwao itakuwa ya kulinda heshima tu.
Lakini Azam tayari imejihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo na hivyo kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
Waliokuwa mabingwa watetezi Yanga, hawana tena chao- kwani hata wakiifunga Simba keshokutwa watabaki nafasi ya tatu tu, hivyo mwakani hawavuki mipaka ya nchi.
Tumaini pekee la Yanga kucheza michuano ya Afrika mwakani ni iwapo Simba SC itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu- ikiwa imebakiza mitihani miwili kufikia mafanikio hayo.
Inatakiwa kuitoa Al Ahly Shandy ya Sudan- na baadaye iitoe timu itakayokutana nayo kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua hiuyo, ambayo itakuwa imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
Hapo, Tanzania itakuwa na nafasi mbili kwenye Kombe la Shirikisho mwakani, kwa mujibu wa kanuni mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Tayari Simba imeifunga Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na inahitaji sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Awadh Issa dakika ya 25, wakati kipindi cha pili, Wakata Miwa hao wa Manungu waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Simba, walipata bao la pili dakika ya 59, mfungaji akiwa ni Juma Abdul.
Awadh alifunga bao lake akiunganisha kona iliyochongwa na nyota wa mchezo wa leo, Juma Abdul ambaye naye alifunga bao la pili kwa mpira wa adhabu, baada ya Luckson Kakolaki kumchezea rafu Vencent Barnabas Saramba.
 
SOURCE: BIN ZUBEIRY (http/bongostaz.blogspot.com)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA