Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam juzi
 Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika  msafara kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao .
Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live
 Naibu Waziri Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani.
 Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012.
Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao.
 Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.
 Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).
Mashabiki wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za ubingwa.
---
TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE. Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi  na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live. Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA