TAHADHARI: Michango inayochangishwa na Mkurugenzi wa Moses Nursery School ya Yombo Vituka, Dar es Salaam, Bw. Moses Kabambara haina uhusiano wowote na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete: IKULU

Katika siku chache zilizopita, Mkurugenzi wa Shule ya Chekechea ya Moses Nursery ya Yombo Vituka, Dar es Salaam, Bwana Moses Kabambara amekuwa anasambaza kadi kwa watu binafsi, makampuni, mashirika na ofisi za ubalozi zilizoko nchini akisaka michango kwa ajili ya ununuzi wa madawati na ujenzi wa madarasa na uzio wa shule yake.

Katika kadi yake ya kuomba michango na kwenye taarifa anazozisambaza kwenye vyombo vya habari, Bwana Kabambara anatumia jina la Mheshimiwa Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nembo ya Taifa kuonyesha kuwa Mheshimiwa Mama Kikwete ndiye mchangishaji na Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya shughuli ya kuchangia maendeleo ya shule yake.

Aidha, amekuwa anadai kuwa Mama Kikwete ndiye atakuwa Mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo.
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuuarifu umma wa Tanzania kama ifuatavyo kuhusu suala hili:

(a)    Kwamba Mama Salma Kikwete kamwe hajapata kuridhia kuwa Mgeni Rasmi katika matembelezi hayo
(b)    Kwamba Mama Salma Kikwete hajapata kukubali kuwa mchagishaji ama hata mshiriki wa aina yoyote katika uchangishaji fedha kwa ajili ya shule hiyo.

(c)    Kwamba Bwana Kabambara anaufanyia udanyifu umma ili uweze kuamini kuwa Mama Salma Kikwete amekubali kushiriki katika shughuli za uchangiaji fedha shule yake.

Tunapenda kupitia taarifa hii kuutahadharisha umma kuwa macho na vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia majina ya Viongozi wa Kitaifa kuchangisha ama kukusanya fedha ama hata kufanya mambo mengine yenye kulenga manufaa au maslahi binafsi.

Hili ni kosa la jinai mbali na kwamba vitendo vya namna hii husababisha usumbufu kwa jamii na kwa viongozi husika.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Mei, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*