TAIFA STARS NA MALAWI KUKIPUTA JUMAMOSI DAR


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Malawi, kinawasili nchini Ijumaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa, Taifa Stars, utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa wameshapata taarifa ya ujuo wa wageni wao hao.

Alisema licha ya kujua siku ya kuja lakini bado hawajataja idadi ya watakaokuja licha ya TFF kuwapa idadi ya watu 27 ambao watakuwa chini yao.

"Tumewaambia wakija 27 ni idadi ambayo itakuwa chini yetu kama watazidi wengine watakuwa chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Malawi"alisema Osiah.Stars iliyopo kambini chini ya kocha Kim Poulsen inacheza mechi kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kwenda kuivaa timu ya Taifa ya Ivory Coast ugenini Juni 2, jijini Abidjan.

 Mechi hiyo ya  mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 kwa kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast . wachezaji ambao wapo kambini kujiandaa na mchezo huo makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar).
Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI