TASWA WAMPONGEZA MHARIRI WA MICHEZO TANZANIA DAIMA

Tullo Chambo

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimatoa pongezi kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT).

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando imesema, Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT uliofanyika Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya walioingia kwenye chama hicho.

Wengine walioshinda ni Anthony Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla, Mhazini, Is-Haq Suleiman.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro, Peter Mwita, Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda, Robert Kalyahe na Christian Matembo.

TASWA inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mhariri wa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi yanayohusu riadha, hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia atakuwa kiongo kizuri kwa waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya riadha.

TASWA inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia kila la heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT waliomuamini wakamchagua kushika wadhifa huo.

Pia Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili, ikiamini watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI