TWIGA STARS UWANJANI ETHIOPIA LEO


Twiga Stars inacheza leo (Mei 27 mwaka huu) na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
 
Mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa saa za nyumbani itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa ulioko jijini Addis Ababa na timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Addis Ababa, wachezaji wa Twiga Stars ambayo imefikia hoteli ya Churchil, leo saa 4 asubuhi wamefanya mkutano wa mwisho wa maandalizi ya mechi hiyo na kocha wao Charles Boniface Mkwasa na baadaye kupata chakula cha mchana kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
 
Twiga Stars; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Evelyn Sekikubo, Mwapewa Mtumwa, Etoe Mlenzi, Mwanahamisi Omari, Ester Chabruma, Fatuma Mustafa na Asha Rashid.

Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said, Semeni Abeid, Zena Khamis, Amina Ally, Rukia Hamis na Fadhila Hamad.
 
Mchezo huo unachezeshwa na Angelique Tuyishime akisaidiwa na Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga wote kutoka Rwanda. Kamishna ni Catherine Adipo kutoka Uganda. (Chanzo; Full Shangwe Blog)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA