VIBANDA VYA NYAMA YA' KITIMOTO' VYAFUNGWA MUHEZA

IDARA ya Afya wilayani Muheza, imevifunga  vibanda vya kuuza nyama choma  ya nguruwe (pichani) kutokana na ugonjwa wa kipindupindu ambao unatikisa wilayani hapa.

 Vibanda hivyo vilifungwa juzi na maofisa  afya wa Wilaya ya Muheza, chini ya ulinzi wa polisi.  Akizungumzia suala hilo, Mratibu wa Shughuli za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wilayani Muheza, Boniface Jacob alisema wameamua kufunga vibanda hivyo kutokana na mazingira machafu ambayo yanaweza kuchochea mlipuko wa kipindupindu. 

Jacob alisema vibanda hivyo havifai kwa biashara ya chakula cha binadamu na kwamba, havijasajiliwa na TFDA.  Alisema hakuna machinjio ya nguruwe wilayani Muheza na kwamba,  nyama hiyo haikaguliwi na mkaguzi wa nyama  wa wilaya.  Mratibu huyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo, nyama hiyo ya nguruwe siyo salama kwa binadamu.

 Alisema mbali ya kipindupindu walaji pia wanaweza kuambukizwa magonjwa kama mafua ya nguruwe, minyoo  na magonjwa mengine hatari.  Jacob alisema  vibanda hivyo vimefungwa mpaka hapo sheria na taratibu za biashara ya chakula cha binadamu zitakapofuatwa.

 Wakati huohuo,watumiaji wa kilaji hicho cha nyama ya nguruwe wameonekana kuhaha kutokana na vibanda vinavyouza nyama hiyo kufungwa.   e&p

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI