WASAMARIA WEMA - LAUREN LAURENT ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA


Bukobawadau Blog tumeshuhudia mdau huyu katika hali hii na  akihitaji msaada  wa matibabu kwa  Mzee Raza wa Izaas Medical Project mjini hapa.
 Wao Izaas na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwasaidia watu wenye shida na wenye magonjwa mbalimbali   na kutoa miguu ya bandia kwa watu wenye ulemavu.

Akiongea na Bukobawadau Mkurugenzi wa Izaas Ndg Raza Fazal anamesa "Takwimu zinaonyesha kuwa Wilaya za Chato na Biharamulo kuna wagonjwa wengi wa Goita na matatizo mbalimbali  hivyo walifanya mpango na kuagiza wagonjwa wapatao 20 kutoka Wilaya ya Biharamulo na wakati wanafika katika ofisi za Izaas Mjini Bukoba kulikuwa na Mgonjwa mmoja wa ajabu sana mwenye uvumbe kichwani ambae ni Ndg Lauren Laurent mwenye miaka 46.

Lauren alipata ugonjwa huu tangu  miaka ya sabini  na kwa kukosa msaada ndio maana hadi leo hii yupo katika hali hii,na tatizo linazidi kukuwa kila siku, na Izaas wamefanya jitiata na kumpeleka katika hospital ya Mugana na kukutana na Dr.Mazima ambae amekubali kuwa anaweza kufanyiwa Upasuaji(operation) pale pale Mugana.

Lakini Madaktari wengi walioko nje ya Nchi wameshauri kwamba ili Operation hii ifanyika panatakiwa awepo Neuron Surgeon(hii ni ngazi flani ya utalamu zaidi) akishirikiana na Dr. Mazima.

Mpaka tunaingia hewani tarifa kamili  ni kwamba Izaas wamefanikiwa kumpata Neuron Surgeon Dr. Nice Rutabasibwa wa muhimbili hospital na amekubali mgonjwa apelekwe pale.

Kwa sasa mgonjwa huyu anahitaji msaada wa Nauli yake yeye na Dr. Mazima wa Mugana,pia gharama za Operation, vipimo vya MRI na matumizi yake akiwa Jijini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi Email izaasmedicalproject@gmail.com AU Simu namba +255714533430 
Kwa Hisani ya Bukobawadau Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.