ZANZIBAR HALI BADO NI TETE MABOMU YA MACHOZI YAENDELEA KURINDIMA 

Hizi ni baadhi ya vurugu zilizotokea jana Mjini Zanzibar huku mabomu ya machozi yakirindima na kuendelea kupigwa na polisi wakati wa vurugu zilizoshababishwa na kundi kubwa la watu kwenda kuvamia kituo cha polisi ili kushinikiza kiongozi wao aliyeshikiliwa na jeshi la polisi aachiwe huru
Picha askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano n awananchi wa zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha za jadi kama vile rungu na mapanga
Hali tete bado inaendelea asubuhi ya leo mjini zanzibar huku polisi wakiwatawanya wananchi wa zanzibar lakini wananchi hao wanazidi kuongezeka kwa kutaka kiongozi wao kuachiwa huru na polisi ambapo alikamatwa jana na wananchi hao kuvamia kituo cha polisi jana jioni na hatimaye polisi kutumia mabomu ya machozi tokeaa jana jioni hadi asubuhi ya leo
Wananchi wa Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi na kabla machozi ya mabomu hayajaanza kulipuliwa na askari.Picha Zote na  Abdulaziz El Shuwehdy

JANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO. Kwa hisani ya Lukaza Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.