AIRTEL YAJA NA KOPA NA UDAKE SALIO

Maofisa wa Airtel kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya “Daka Salio” wakati wa uzinduzi Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Moroco na kuhudhuria  na waandishi wa habari, kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano na Matukio, Bi. Dangio Kaniki, Meneja Uhusiano, Jackson Mmbando na Meneja Bidhaa, Salim Madati.
*********************
 - Salio la mkopo kutumika kupiga mitandao yote nchini

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuendeleza dhamira yao ya Uhuru wa kuongea imetoa fulsa nyingine kwa wateja wake kwa kuzindua huduma kabambe ya Daka salio ikiwa ni jitihada zake katika kutimiza dhamira yake ya kuendelea kutoa uhuru wa kuongea kwa wateja wake nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando by Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kuleta huduma hii ya Daka salio kwa wateja wetu wote waendelee kufurahia huduma zetu kila wakati, ikiwa sasa unaweza kukopa na kuongea na ndugu au rafiki wa mtandao wowote sasa hakunakubeep tena.
Hii ni huduma nzuri kwa familia, marafiki ndugu au jamaa kwa kuwa itaondoa tatizo la watu kubeep, Airtel tunasema kwanini ubeep au uteseke kukopa kiwango kikubwa na kulipa zaidi.  Daka salio kidogo na ulipie kidogo na airtel. Ili kufurahia huduma hii ni rahisi na haraka tuma tu neno daka kwenda 15549.  Uongee mwanzo mwisho, kwa raha zako.
Mteja yeyote anaweza kukopa ikiwa tu amekuwa mteja wa Airtel kwa mfululizosiku tisini, awe anasalio la hadi shilingi 50 na asiwe anadaiwa deni la Daka salio ikiwa alishakopa kupitia huduma hii.
Faida ya kukopa salio ya Airtel ni kwamba tunakukopesha kiwango kidogo ambacho utalipia kiduchu tu na utaongea kwa muda mrefu. Achana na wanaokopesha kiwango kikubwa halafu unaongea kidogo.
Mteja wa Airtel anaekopa salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na akitaka kulipa atalipa ziada ya sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu, kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500 bado utabakia na salio la kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel.
Airtel  imekuwa na ubunifu wa bidhaa na huduma zake zaidi  kwa lengo la kufaidisha jamii kwa ujumla. Hivi karibuni ilizindua huduma ya SUPA 5 yenye dili tano bomba na inaendelea kutoa unafuu kwa wateja wa Airtel kupata sms 200 bure, kuongea na watu watatu kwa nusu shilingi siku nzima,  kupata huduma ya facebook bure , intaneti bure usiku, pamoja na kongea kwa robo shilingi nyakati za usiku kwa kupiga tu *149*99# na kufuata utaratibu.
Airtel pia kupitia huduma yake ya Airtel money inawawezesha wajasiliamali waliowekeza katika kwa kuwa wakala wake nchi nzima pamoja na wateja wake,  kwa wateja sasa wanapata  mara mbili ya salio wanaloongeza kupitia huduma ya Airtel Moneywakati  WAKALA wote nchi nzima watapata mara mbili ya kamisheni zao kwa mwezi juni - julai kwa mihamala yote watakayofanya kupitia Airtel Money.Chanzo;Daily Mitikasi Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.