Ajali ya Zanzibar si Upepo Mkali

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kuwa ajali ya meli iliyotokea Zanzibar haijasababishwa na upepo mkali kama inavyoelezwa.

Mkurugenzi wa taarifa za utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa, aliliambia gazeti hili jana kuwa huenda ajali hiyo imetokana na sababu zingine, kwani kama ungekuwa upepo ni wazi kuwa meli, boti na mitumbwi iliyopo kwenye Bahari ya Hindi vingezama au kupeperushwa.

“Siwezi kuitaja sababu ya ajali ya juzi, isipokuwa naweza kusema kuwa upepo ulikuwa wa kasi ya kilometa 30 hadi 40 kwa saa,” alisema.

Kwa mujibu wa maelezo yake, upepo wa juzi ulikuwa mkali kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi na kusababisha vumbi na mawimbi juu ya bahari hiyo.

Alisema kwa jana walitarajia upepo mwingine wenye kasi ya kilometa 20 hadi 30 kwa saa kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi, lakini hali ikawa tofauti.

Hata hivyo, aliongeza kuwa kutokana na hali ya hewa kwa siku mbili hizo kuwa tete hali sasa ni shwari.

Kutokana na maafa ya Zanzibar, TMA ilitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini kupata taarifa za mara kwa mara za mwenendo wa hali ya hewa.

Alisema hatua ya kupata taarifa za mara kwa mara zitasaidia kwa kiasi kikubwa kufahamu hali ya hewa na mwenendo wa upepo kwa siku husika kabla ya safari zao.
Chanzo: Tanzania Daima Julai 20.2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU