BENDI YA EXTRA BONGO YAZINDUA RASMI UKUMBI WAKE WA NEW WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE

Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akiimba jukwaani mbele ya mashabiki lukuki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wao mpya New White House, utakaojulikana kwa jina la 'Bongo Resort Kimara Korogwe' wakati wa onyesho maalum la uzinduzi wa ukumbi huo lililofanyika jana. Extra Bongo  walizindua ukumbi huo mpya wa New White House a.k.a Bongo resort uliopo kimara Korogwe, ambapo uzinduzi huo ulisindikizwa na kundi la bendi ya Taarabu ya Coast Modern Taarab, iliyo chini ya Omary Tego na Maua Tego, na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama, Tunda Man, Sheta na kundi maarufu la BAIKOKO kutoka Mkoa wa Tanga.
Rogert Hegga. 'Katapila' akiimba jukwaani wakati wa onyesho hilo katika ukumbi wao mpya uliopo Kimara Korogwe Dar es salaam.
Ally Choki (kushoto) akipozi na mdau Henry.
Mnenguaji mahiri wa Extra bongo akishambulia jukwaa.
Wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo, Danger Boy (kushoto) na Super Nyamwela, wakishambulia jukwaa.
Jembe la Extra Bongo Banza Stone A.K.A Makaveli, akipagawisha wapenzi wao ndani ya White Inn Kimara Korogwe.
Mwanamuziki wa BAIKOKO akishambulia jukwaa ikiwa ni sehemu ya kusindikiza uzinduzi huo uliofanyika jana.
Tunda Man naye hakuwa nyuma katika kuwaburudisha mashabiki wa Extra Bongo.
Mwanamuzi wa Kizazi kipya Bongo Fleva Sheta, akiwakimbiza washabiki wake ndani ya ukumbi mpya wa Extra Bongo katika uzinduzi wa ukumbi huo. Chanzo; Sufiani Mafoto Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*