BENDI YA MASHUJAA YAZINDUA VIDEO YA RISASI KIDOLE

 Rais wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wanakebega'  Charles Gabriel 'Chalz Baba' (kulia) na Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter wakionesha DVD ya video yao mpya iitwayo 'Risasi Kidole' wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Video hiyo ina nyimbo za Ungenieleza, Hukumu ya mnafiki, Kwa mkweo, Baba Isaya, Umeninyima na Thamani ya Mtu.PICHA NA KAMANDA MWAIKENDA
                                                      Wanamuziki wa bendi hiyo wakifanya shoo
 Meneja wa Bendi hiyo, Martine Sospeter, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Chalz Baba
                                         Charlz Baba (kulia) akizungumza katika mkutano huo
                                                     Wanahabari wakiwa kazini katika tukio hilo
 
Na Asha Kigundula

RAIS wa bendi ya muziki wa dansi nchini Mashujaa Wanakebega' Charles Gabriel Chalz Baba' amewataka wapenzi wa muziki nchini waipokee kazi yao mpya itakayozinduliwa hivi karibuni.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wakitambulisha video yao mpya iitwayo Risasi Kidole, Chalz Baba alisema kuwa wamejipanga vizuri kwa kuanza na kazi hiyo ya Risasi Kidole ambayo imeshakamilika.

Chalz Baba alisema kuwa tayari wameshafyatua video mpya, ya wimbo Risasi Kidole, ambayo itazinduliwa baada ya mfungo wa mwezi mtukufutu wa Ramadhani.

Alisema kuna baadhi ya watu walisema wao wamekwenda kwenye bendi hiyo kama utalii wakiwa hawajui nini kinachoendelea.

"Sisi tumekuja kazini nia yetu ni kuleta burudani lakini kuna watu walikuwa wanasema kama sisi tumekuja kucheza sasa ndiyo wataona tunafanya nini kwa kuanza na kazi hii ya kwanza

Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter amesema video hiyo itaanza kuonekana kwenye vituo mbaolimbali vya Televisheni nchini kote, wakati wowote kuanzia sasa.

Alisema kuwa licha ya kutoa wimbo huo kuna nyimbo nyingine tayari zimeshakamilika na zinatarajia kutoka hivi karibuni.

Sospeter alisema hapo awali walikuwa wamepanga kufanya utambulisho wa wimbo huo kesho wameamua kusogeza mbele ili hata waislam waweze kushuhudia utambulisho huo.

Alisema sababu kuu ya kughairisha ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao utaanza kesho au kesho kutwa.

Licha ya kuzungumzia wimbi huo Sospeter alisema kuwa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani bendi hiyo itakuwa inafanya burudani kama kawaida isipo siku ya Jumatano.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.