Dk Rotich kufungua mafunzo ya Wapigapicha kesho Arusha


NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich (pichani) anataraji kufungua mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yatakayo anza Julai 23-26, 2012 mjini Arusha.

Juma la wapigapicha 10 kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki wanataraji kuhudhuria mafunzo hayo ya siku tatu ya Upigaji yatakayofanyika katika Hotel mjini Arusha.

Mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jumuia ya Afrika Mashariki na Shirika la Kijerumani (EAC) na  GIZ yatahusiha wapigapicha hao kumi, wawili kutoka kila nchi.

Tanzania inawakilishwa na Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti na Habari za Mtandao, Mroki Mroki, Mwasisi na Mhariri Mkuu wa FATHER KIDEVU BLOG pamoja na Mwandshi wa Kampuni ya Mwanachi Comunication mjini Arusha, Filbert Rweyemamu.

Tayari wapigapicha hao wa Habari wapo mkoani Arusha wakiwasubiri wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuwasili kwa kuanza mafunzo hayo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ni Balozi wa Heshima wa Utalii nchini Kenya na Mwenyekiti wa mfuko wa 50 Treasures of  Kenya, Hartmut Fiebig.Chanzo Father Kidevu Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA