DK ULIMBOKA AZUSHIWA TENA KIFO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka ambaye alitekwa, kupigwa na kutupwa Mabwepande, Dar es Salaam, amezushiwa kuwa amefariki dunia.

Dk. Ulimboka ambaye, hivi karibuni madaktari wenzie walichanga fedha na kuamua kumpeleka kwenye matibabu Afrika Kusini, amezushiwa na watu wasiojulika kuwa amefariki hasa baada ya asubuhi kupata taarifa Radio BBC, kuwa hali yake ni mbaya.

Watu walikuwa wanatumiana meseji kuhusu uvumi huo, hali ambayo imesababisha taharuki kwa watu mbalimbali wakiwemo madaktari .

Wengine walidiriki kusema kuwa madaktari Muhimbili wameandamana baada ya kusikia taarifa za kifo hicho, jambo ambalo si kweli.

Kamanda wa matukio iliamua kuwasiliana kwa njia ya simu na baadhi ya madaktari Hospitati ya Muhimbili, lakini wengi wao walikanusha habari hizo.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA