DR. ASHA ROSE MIGIRO AREJEA NCHINI.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.
Pichani juu Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.

Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.

Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.

Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.

Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.

Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA