MTANZANIA ANAYEISHI MAREKANI ASIFU HUDUMA ZA NSSF WESTADI


Bernadeta Kaiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau akipeana mkono na Bernadeta Kaiza ambaye alifika katika banda la NSSF kutoa ushuhuda wake pamoja na kuishukuru NSSF kwa kugharamia  safari ya kusafirisha mwili wa marehemu mume wake ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTADI aliyefariki nchini ns kusafirishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutoka marekani mpaka Tanzania kwa ajili ya mazishi. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walipofka katika banda la NSSF katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam.
Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Bernadeta Kaiza akiwashukuru Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada NSSF kusafirisha mwili wa marehemu mume wake ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTADI, aliyefariki nchini Marekani hivi karibuni na Kuzikwa Tanzania ambapo NSSF iligharamia safari yote ya kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi.
 Bernadeta Kaiza (kushoto) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa  Bodi ya wakurugenzi wa NSSF.

DAR ES SALAAM Tanzania,

Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Bernadeta Kaiza ametoa wito kwa watanzania wanaoishi ughaibuni  kujiunda na mafao ya Welfare Scheme  for Tanzanian Diaspora (NSSF WESTEDI) huduma ambayo itamuwezesha mwanachama kupata huduma ya kusafirishwa kutoka nchi husika mpaka nyumbani Tanzania pindi anapofariki.

Akizungumza katika banda la NSSF  mbele ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) waliofanya ziara katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

"Kujiunga NSSF WESTEDI kutasaidia mwanachama kugharamiwa safari ya kusafirisha mwili kutoka nchi yoyote mpka Tanzania na kuondokana hali ya kuchangihana fedha pindi mmoja wetu anapofariki."

Wakati mwingine tunashindwa kusafirisha mwili kutokana na kukosa fedha lakini kwa kupitia huduma hii ya NSSF WESTEDI sasa matatizo ya muda mrefu tuliyokuwa nayo sasa yatakwisha endepo watu wengi watajiunga na huduma hii kutokana na gharama zote za mwanachama kugharamiwa na NSSF, aliongeza Bi. Bernadeta Kaiza wakati akiishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF kwa kufanikisha safari ya kuja Tanzania pamoja na mwili  wa marehemu mume wangu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifandhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Kitwana Dau amesema kuwa  ili kujiunga na mafao hayo mwanachama anatakiwa kutoa ada ya uanachama ambayo ni Dola za Marekani 300 kwa mwaka na fomu zinapatikana katika mtandao.


NSSF WESTADI
Mpango wa Ustawi kwa Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi. (WESTADI)

NSSF sasa imepanua huduma zake kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia mpango maalum kwa wanaoishi nje ya nchi iutwao WESTADI, yaani Mpango wa Ustawi kwa Watanzania Wanaoishi Ncje ya Nchi.

Lengo ni la bima hii ni kufidia Watanzania wote wanaoishi nje ya nchi (ikiwa ni pamoja na Wanafunzi) ikiwamo kuchagua wategemezi wanne wa kuwawekea bima hii (wanaoishi nje) kupitia Faida ya Bima ya Afya kwa Jamii (SHIB) hapa Tanzania

FAIDA ZA MFUKO

  1. Huduma ya afya nchini kwa wategemezi wanne
  2. Kama Mtanzania anayeishi nje atakuja Tanzania na mke wake au mwenyewe na kupata maradhi, bima hii inaweza kutumika hapo
  3. Kama mtu atakufa ughaibuni wanatoa tichecket ya msindikizaji, Wanalipa utunzaji wa maiti na wanasafirisha mwili mpaka Tanzania

MASHARTI

Bima (kwa anayeishi nje ya nchi) itatokana na mchango wake wa kiasi cha pesa kwa mfuko

KIWANGO

Kiwango cha kusanyo la bila ni Dola za Marekani 300 kwa mtu mmoja aliyeko nje

MAHITAJI YA HUDUMA
Huduma ya Bima ya Afya

Mtegemezi atachagua hospitali iliyo ndani ya mkoa husika na huduma kwake zitaanza mara moja baada ya kuthibitishwa kwa ingizo la pesa za Bima ya Mtu aliyeko nje.

Wategemezi kutembelea ofisi ya karibu ya NSSF kote nchini kwa ajili ya mchakato wa usajili wa Bima ya Afya

Huduma zitasimama mara punde mwenye bima atakapositisha na kuondoa michango ya pesa za kila mwak.Chanzo; Habari Mseto Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.