JK AWAKARIBISHA WACHINA KUWEKEZA NCHINI

RAIS Jakaya Kikwete ametoa wito kwa Wachina kuja nchini kuwekeza katika kilimo kwa kuwa Tanzania imebahatika kuwa na ardhi yenye rutuba.Alisema sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kilimo nchini na kwamba wawekezaji wa ndani wakishirikiana na wenzao wa China kilimo kitakuwa na mafanikio makubwa.

Rais Kikwete alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kimataifa kuhusu mageuzi ya kilimo kwa maendeleo na kuondoa umaskini Afrika.Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (POPC) kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Kuondoa Umaskini cha China (PRCC), Kikwete alitaja Mikoa ya Iringa, Mbeya Ruvuma, Rukwa na Morogoro kuwa ndiyo yenye mazingira mazuri kwa kilimo.

Rais Kikwete aliwaambia wajumbe 120 wanaohudhuria kongamano hilo kwamba bila sekta binafsi kuwekeza katika kilimo, vita ya kupambana na umaskini itakuwa ngumu hapa nchi na Afrika kwa ujumla.  “Sekta binafsi inaweza kuwekeza katika kilimo cha mashamba makubwa, kuuza vifaa vya kilimo, kutoa mikopo kwa wakulima, utafutaji wa masoko ya mazao na kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao,” alisema Kikwete.

Alisema sekta binafsi ikifanya hayo, Serikali kazi yake itakuwa ni kuimarisha miundombinu kama vile barabara ili kuweka mazingira bora ya kilimo na upatikanaji wa masoko.“Siku za nyuma sekta binafsi haikutumika katika kilimo, lakini hivi sasa tumejipanga kuona kwamba wanakuwa wadau wakubwa,” alisema Kikwete.
Alisema sababu mojawapo inayokwamisha kilimo hapa nchini ni kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kilimo kwa sababu wakulima wengi ni maskini wasiokopesheka na benki.Kikwete aliiomba Serikali ya China kuisaidia Tanzania katika eneo la utafiti wa kilimo ili kupata mazao yenye ubora zaidi na hivyo kuwaletea manufaa wakulima.   

Naye Waziri wa Nchi, Maendeleo  na Kuondoa Umaskini wa China, Fan Xiaojian alisema kilimo nchini mwake kilifanikiwa baada ya kuwawezesha wananchi wa vijini kielimu na kiuchumi.Alisema Wachina walifundishwa namna ya kuendesha kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ambazo waliwezeshwa kuwa nazo huku wakifanya hayo kwa kushirikiana.

Xiaojian alisema Serikali iliwekeza kwenye tafiti za kilimo kwa kuvipatia vyuo vya kilimo vifaa na fedha za kutosha kufanya shughuli zake.Naye Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dk Philip Mpango alisema lengo la kongamano hilo ni kubadilishana uzoefu kati ya China na nchi za Afrika katika maendeleo ya kilimo na upunguzaji wa umaskini.

Alisema pia ni kuangalia namna nchi za Afrika zinavyoweza kufaidika na maendeleo yaliyopatikana China.Kwa mujibu wa Dk Mpango, mbali na wataalamu wa Kichina walioshiriki  katika  kongamano hilo, nchi nyingine ni Tanzania, Kenya, Zambia, Ghana, Senegal, Siera Leon, Eritrea na Mauritius.

Lengo la kongamano hilo ni kuchanganua kilimo cha kisasa cha China na kuangalia uwezekano wa ujuzi huo kutumika katika sekta ya kilimo katika nchi za Afrika.Ajenda zinziojadiliwa niu mtazamo mzima wa maendeleo ya kilimo na upunguzaji umaskini na China na Afrika, wajibu wa kilimo na teknolojia ya kilimo, tafiti na kuongeza huduma katika kilimo cha kisasa.Kongamano la tatula ushirikiano wa kimaendeleo la upunguzaji wa umaskini

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU