KAMBI YA ILALA YAENDELEA KUMFUA BONDIA IBRAHIMU CLASS

Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli katikati akiwaelekeza mabondia Yohana Robert KUSHOTO NA Ibrahimu Class jinsi ya kutupa masumbwi kwa mpizani kwa kunyoosha mkono Class anajiandaa na mpambano wake na Simba Watundulu siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es salaam.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class kushoto akipambana na Yohana Robart wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambnano wake na Simba Watundulu utakaofanyika siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond JubleePicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 Na Mwandishi Wetu

KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu

Class 'Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60

litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond Jublee

Akizungumza mmoja wa makocha wa kambi ya ilala inayongozwa na Kocha mkongwe wa

mchezo huo Habibu Kinyogoli, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema katika kipindi

hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wanamwandaa bondia Ibrahimu Class kwa ajili

ya mpambano huo utakaofanyika siku hiyo


Super D alisema wamemuandaa bondia wao kufanya vizuri hili kuweza kumzibiti

mpinzani wake kwa kuwa wanamjua uchezaji wake awapo ulingoni hivyo wanamfundisha

mbinu mpya kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake

Kambi hiyo ya ngumi imewataka wadau wa mchezo uho kuja kuangali mchezo mzuri wa

masumbwi utakaoneshwa na bondia wao kutoka kambi ya ilala

Ibrahimu Class anaetamba kwa jina la Ibra Mawe yupo chini ya maandalizi makali

chini ya makocha wake Kinyogoli na Super D kwa ajili yampambano huo na kuwataka

wapinzani wake kwa sasa wakae chonjo kwa kuwa moto umesha washwa na akuna wa

kuuzima kwa bondia huyo chipkizi na mwenye nia ya kuupaisha mchezo wa masumbwi

Kimataifa mabondia hawo watakuwa wakicheza katika mpambano wa utangulizi wa

RAUNDI 6 uku pambano kuu ni kati ya Ramadhani Shauli wa Tanzania na Sande Kizito

wa Uganda watakaopambana kugombania mkanda wa Ubingwa wa IBF se3sAfrika

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*