MARUFUKU MWANAFUNZI KUGUSA CHAKI

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akiongea na wakuu mbalimbali wa elimu mkoani Mbeya


WALIMU waliozoea kuwapa chaki na notsi wanafunzi ili wakawaandikie wenzao madarasani sasa watawajibishwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi watakapobainika.

Naibu waziri wa wizara hiyo Filipo Mulugo ametoa agizo hilo katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa idara ya elimu kanda,mkoa na wilaya pamoja na wakuu wa shule za sekondari za mkoani Mbeya na wakuu wa shule za msingi katika halmashauri ya jiji.

Kadhalika Mulugo amekataza mamonita wa madarasa kuitisha majina ya mahudhurio ya wanafunzi wenzao akisema mwenye jukumu hilo ni mwalimu wa darasa husika na itakapobainika mwalimu huyo pamoja na mkuu wa shule husika watawajibishwa.

Amesema shughuli zote hizo si za mwanaafunzi na zinazorotesha ufanisi katika utendaji kwakuwa walimu wanakaimisha majukumu hayo na wao wakibaki wanapiga soga ofisini mwao na walimu wenzao.Chanzo;Mbeya Yetu Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI