MIKOA MITANO YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NA PESA ZA POOL SAFARI LAGER TAIFA

Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Jafari Michael (kushoto) akicheza kuashilia ufunguzi rasmi wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa katika klabu ya Makanyaga Mkoani Kilimanjaro.
Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Jafari Michael (kuli) akimkabidhi t-shirt na pesa nahidha wa timu ya Makanyaga wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Safari Pool ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro.
DAR ES SALAA, Tanzania.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager leo imekabidhi vifaa vya michezo katika mikoa mitano inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza leo katika mikoa hiyo
Vifaa hivyo t-shirt pamoja,pesa za nauli kwa kila timu na pesa za zawadi kwa timu zitakazoshinda katika fainali za mikoa hiyo ambazo wamekabidhiwa manahodha wa kila klabu shiriki.
Mikoa iliyokabidhiwa vifaa na pesa hizo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Manyara,Tabora na Kagera.
Makabidhiano hayo yalifanywa na wageni rasmi mbalimbali kila Mkoa ambapo Tabora alikuwa Ofisa utamaduni wa Wilaya, Mark Katunzi,Shinyanga alikuwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya, Asha Mbwana, Kagera alikuwa, Ibrahim Mabruk, Manyara alikuwa, Ofisa Elimu ya Watu Wazima, Fausta Akoro na Kilimanjaro alikuwa Jafari Michael ambao kwa ujumla waliwataka wachezaji wa Pool kuuheshimu mchezo na kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha mashindano na watambue kuwa kwenye mashindano lazima apatikane mshindi wa kwenda kushiriki Taifa kuuwakilisha Mkoa.
Aidha waliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kufadhili mashindano hayo kwani yanawafanya vijana faidike na kiasi cha fedha wanachoshindania licha ya burudani waipatayo ambayo inawaepusha na mambo mengi yasiyo na faida mtaani
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kesho na kumalizika Julai 8 mwaka huu ambapo timu itakayoibuka bingwa kwa upande wa Mkoa itajinyakulia kitita cha sh. 700,000 huku mchezaji mmoja mmoja akiondoka na sh. 350,000 kwa upande wa wanaume na wanawake wa kwanza atazawadiwa sh. 250,000 taslimu.
mshindi wa pili kwa upande wa timu, atazawadiwa sh. 350,000, mshindi wa tatu, 200,000, wa nne sh. 100,000 na kifuta machozi cha sh. 50,000 kitatolewa kwa timu zitakazoshiriki.
Halikadhalika kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume mshindi wa pili atapata sh. 200,000, wa tatu sh. 150,000 na wa nne sh. 100,000 ambapo wanaume kwa wanawake wanne kati ya wanane watakaopoteza mchezo katika awamu ya pili watazawadiwa sh. 50,000, na wakataopoteza katika awamu ya kwanza wanane kati ya 16 wataambulia sh. 20,000.
Aidha kwa upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja mshindi wa pili atazawadiwa sh. 150,000, wa tatu sh. 100,000 na wa nne ataambulia sh. 50,000

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA