Misri: Mahakama kujadili amri ya rais

Mahakama Kuu ya kikatiba nchini Misri ambayo mwezi uliyopita ilitangaza amri ya kuvunjwa kwa bunge la nchi hiyo inatarajiwa kujadili hatua ya Rais Muhammed Murisi ya kutangaza bunge liendelee na shughuli zake.
Spika wa bunge hilo tayari ametangaza kuwa wabunge wakutane siku ya Jumanne kwa vikao vya bunge.
Wakuu wa jeshi na maafisa wa mahakama wamefanya vikao vya dharura lakini hadi sasa hawajatoa uamuzi wowote.

Rais Mursi, ambaye chama chake cha Muslim Brotherhood kilishinda viti vingi amesema bunge lazima liendelee na vikao vyake wakati uchaguzi mpya ukiandaliwa.

Lakini kufikia sasa jeshi bado limezunguka bunge hilo na haijulikani ni lini au vipi wabunge hao watakutana na kuendelea na vikao vyao.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo Jon Leyne anasema kwamba itabidi wabunge hao wafanye bidii ili wauvunje ukuta wa polisi na jeshi ambao uko nje ya majengo ya bunge kabla ya wao kufaulu kuingia ndani au basi itawabidi wakutana kwengine.

Baraza kuu la kijeshi ambalo hivi karibuni lilitangaza kuwa limejitwika mamlaka ya bunge lilifanyaka kikao cha dharura muda mfupi tu baada ya Rais Mursi kutua amri ya bunge kukutana.
Baraza hilo linatarajiwa kufanya kikao chengine tena.

Jeshi lilijitwika madaraka likikidai kwamba lilikuwa tekeleza amri ya mahakama kuu ambayo ilivunja bunge kufuatia malalamiko kuhusu viti vilivyotengewa wagombea huru.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*