MISS UTALII KAGERA KUFANYIKA JUMAMOSI 14-7-2012

Wednesday, July 11, 2012
Shindano la kumsaka Miss Utalii mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika ukumbi wa Linas Club siku ya tarehe 14-7-2012 kuanzia saa, mbili usiku. Katika shindano hilo Warembo 15 watachuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera, ambapo watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu,kitalii,kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni,urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla. Burudani mbalimbali za Ngoma za asili, bendi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakuwepo, wakiwemo Diamond Musica Band, Agcox Burchaman toka Uganda,Maua na BK Sunday. Shindano hilo limedhaminiwa na Cargo Star, Vodacom Tanzania,Kroyera Tours,Vission Radio,Kasibante Radio, prins Hotel,Paradise Hotel,Linas Club ,Mice and Lovely Salon,misstourismorganisation.blogspot.com na Amazing Tanzania Tours(Tours and Safaris) .
Washindi wa shindano hilo watawakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi, na baadae katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012 zitakazofanyika siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanzania 8-12-2012.
Miss Tourism Tanzania  Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"

Mawasiliano zaidi:
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*