Mkurugenzi Global Publishers ashangazwa na mwanamuziki Jose Chameleone

MKURUGENZI wa Global Publishers, Erick Shigongo amewataka Wasanii kuacha tofauti zao katika kutetea maslahi ya nchi na si vinginevyo.
  Kauli hiyo ilitolewa jana, na Mkurugenzi huyo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuzulumiwa dola 3500 na msanii wa Uganda Jose Chameleone.
 Alisema ameshangazwa na baadhi ya Watanzania kumchafua kwenye mitandao kwa kitendo chake cha kumdai msanii huyo wa Uganda, fedha walizokubaliana katika mkataba ili kufanya onyesho la Tamasha la Usiku wa Matumaini.
 Shigongo alisema huu ni wakati kwa watanzania kufahamu ukweli kuhusu hilo kutokana na ukweli kwamba msanii huyo, amekiuka makubaliano ya mkataba wa kwanza ambao walikubaliana kufanya onyesho hilo ghafla akageuka kudai fedha zaidi.
 Alisema hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikubali kuingia mkataba mwingine kwa mara ya pili kutokana na ukweli kwamba alikwishafanya matngazo kuwa msanii huyo angekua mmoja wa wasanii ambao wangefanya onyesho katika tamasha hilo.
 “Kweli tulikubaliana mkataba mwingine nikamlipa dola 8000 na kweli alikuja akafanya onyesho lakini baada ya hapo ndipo nilipomdai fedha zangu dola 3500 alizochukua katika makubaliano ya awali”alisema Shigongo.
 Shigongo alisema si kweli kwamba alizuia pasipoti ya msanii huyo wakati alipokuwa amepangisha chumba kwenye hoteli yake bali kilichotokea ni msanii huyo kuondoka mwenyewe baada ya kudaiwa fedha hizo.
 Katika hatua nyingine, Shigongo alisikitishwa na kitendo cha msanii huyo akishirikiana na vijana wenzake kuvamia ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kwa madai ya kudai kurudishiwa pasipoti yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.