MWANDISHI MWANDAMIZI WA MICHEZO AFARIKI DUNIA

Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo, Chris Mwambonda amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Marehemu Mwambonda, Mawazo Lusonzo.  

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na mipango ya maziko inafanyika nyumbani kwa mama yake mzazi Goba na mipango ya mazishi inafanyika huko huko, taarifa zaidi zitatolewa baadaye. 

Pichani ni moja katika ya matukio aliyoshiriki enzi za uhai wake ambapo hapa anaonekana akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo yaliyowashirikisha wahariri wa michezo na Mkurugenzi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leonard Thadeo baada ya semina ya wahariri wa michezo iliyofanyika Juni 10 2010. 


Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Ameni.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA