MWANZA, ARUSHA, LINDI NA MOROGORO WAKAMILISHA MASHINDANO YA SAFARI POOL TAIFA NGAZI YA MIKOA


 
Mchezaji wa Pool wa Klabu ya Jaba ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Said Mohamed akicheza wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa  kwenye Ukumbi wa New Mwinjuma Dar es Salaam jana.
Mchezaji wa Pool  wa Klabu ya Jambo Lee ya Kinondoni akicheza wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Pool wa Klabu ya Jaba ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Haji Hussein akicheza wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa kwenye Ukumbi wa New Mwinjuma Dar es Salaam jana.
Wachezaji wa Klabu ya Meeda wakimlalamikia mwamuzi, Leodger Masawe wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa wa Kinondoni kwenye Ukumbi wa New Mwinjuma Dar es Salaam jana.
Mchezaji wa Pool wa Klabu ya Shoko ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Modester David akicheza wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa  kwenye Ukumbi wa New Mwinjuma Dar es Salaam jana.

DAR ES SALAAM, Tanzania

MIKOA minne inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mikoa imekamilisha mashindano hayo na  kupata wawakilishi wa mikoa hiyo katika mashindano hayo ngazi ya ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika Septemba jijini Mwanza.

Mkoa wa Mwanza
Klabu iliyotwaa ubingwa ni Paseansi ambayo itawakilisha mkoa wa huo katika Mashindano ya Taifa yatakayofanyika mkoani humo na kwa wachezaji mmoja mmoja (singles) wanaume ni Massen Hassan na kwa wanawake ni Shamira Mohamed. Fainali za Mkoa huo zilihudhuliwa na mgeni rasmi ambaye ni Ofisa Mauzo wa TBL Mkoa wa Mwanza, Bernard Issaria.

Mkoa wa Lindi
Klabu ya Sabasaba ndio itawakilisha mkoa huo na Said Omary atauwaaakilisha kwa upande wa wanaume, Chedi Mages wa klabu hiyo akitarajia kuuwakilisha mkoa upande wa wanawake. Fainali za Mkoa huo zilihudhuliwa na Ofisa Utamaduni wa Manispaa ya Lindi.

Mkoa wa Morogoro
Bingwa ni klabu ya Anatory na mchezaji wa ‘singles’ wa kiume atakuwa ni Athuman Suleman na wa kike ni Rosemary Deus. Mgeni rasmi katika mashindano hayo Morogoro alikuwa diwani wa Kata ya Kingo, Fidelis Tairo.

Mkoa wa Arusha
Mabingwa ni klabu ya 2Eye ambao ndio watawakilisha mkoa wa huo kwenye mashindano ya Taifa jijini Mwanza.

Dar es Salaam
Bado hawajamaliza lakini mikoa mitatu yote ya kimichezo (Ilala, Kinondoni na Temeke) wamefikia hatua ya robo fainali ambapo mara baada ya mfungo wa Ramadhani ndipo wataendelea tena.

Zawadi
Mshindi wa kwanza kwa timu imejinyakulia shilingi 700,000, ya pili 350,000, ya tatu 200,000, ya nne 100,000 na timu zilizobaki zilipewa kifuta jasho cha shilingi 50,000 kila moja.

Singles wanaume bingwa alipata shilingi 750,000 wa pili 200,000, wa tatu 150,000 na wa nne 100,000. Kwa upande wa wanawake bingwa alipata 250,000, wa pili 150,000,wa tatu 100,000 na wa nne shilingi 50,000.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI