NAPE: MZEE SABODO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO

Friday, July 6, 2012
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicheka na
viongozi wa Chadema,  Dk. Slaa na Mbowe hivi karibuni
"Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.
       Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.
       Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote haya yamefanywa na serikali ya CCM.
      Sasa kama serikali ya CCM imefanya hivyo, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya hivyo ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!
     Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!
     Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!"  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika taarifa yake..

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI