NDUGU ZANGU WALIOPOTEA KWENYE AJALI YA MELI NI HAWA HAPA. Inauma sana kwani ukizingatia kwamba nimeagananao asubuhi nakuwatakia safari njema wao wakielekea bandarini nami nikielekea mitaani kutafuta habari.

Huyu hapa anaitwa Chande Abdallah mtoto wa dadaangu ambaeye tukikua tukionekana kama mapacha kutokana na kukaa pamoja miaka mingi, tumesoma shule moja kuanzia Primary hadi sekondari tukiwa Kilwa. Tulihamia Zanzibar tkiwa wote kwa takribani miaka mitano kabla mimi sijaamua kuja kuishi Dar es Salaa. Alifanya ziara Kilwa baada ya kukaa Zanzibar kwa miaka mingi hapa pichani akiwa Kilwa kwnye picha na mtoto wa dadayake. Kimsingi alipiga picha nyingi na watu tofautitofauti jambo ambalo haikuwa kawaidayake kwenda na kamera wala hakuwa nakawaida ya kukaa na picha hata siku moja. Alikua siku zote akiniambi kwamba mimi siwezi kutunza picha nyumbani hata moja sina zinapotea.
Baadi ya picha alizopiga akiwa Kijijini Pande Kilwa ndani ya Mwezi huu wa saba, kabla ya kufikwa na janga la kuzama baharini inauma sana jamani.

Hapa akiwa kwenye picha ya pamoja na wapwaze yaani watoto wa dada zake.
Huyu ni Mtoto wa dadangu mwengine aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo anaitwa Zainabu Abdallah. Picha hii ni ya sikumoja kabla hajasairi akiwa kwenye sherehe ya harusi hapa jijini Dar es Salaa wakiwa wameongozana na kakake Chande kuelekea Zanziba.
Dada huyu nae ambaye waliongozana na Zainabu kuja kwenye harusi jijini Dar es Salaam kuja kwenye harusi naye alikuwemo kwenye ajali hiyo. Kati ya hawa wote hakuna hata aliyepatikana akiwa hai wala kuonekana mwili wake. Kwa hisani ya Raha za Pwani Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA