Skip to main content

ROBO FAINALI COPA COCA-COLA 2012



Robo Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayokutanisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 inaanza kesho (Julai 10 mwaka huu) kwa timu nne kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salam.
 
Temeke na Mjini Magharibi ndizo zitakazocheza robo fainali ya kwanza kuanzia saa 2.30 asubuhi. Mara iliyoivua ubingwa Kigoma itacheza robo fainali ya pili dhidi ya Morogoro kwenye uwanja huo huo.
 
Robo Fainali ya tatu itachezwa keshokutwa (Julai 11 mwaka huu) kwa kuzikutanisha timu za Kinondoni na Mwanza. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi na kufuatiwa na nyingine kati ya Dodoma na Tanga itakayoanza 10 kamili jioni.
 
Nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Juni 24 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikishirikisha timu 28 itafanyika Julai 13 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
 
Mshindi wa mechi kati ya Temeke na Mjini Magharibi, na Kinondoni dhidi ya Mwanza ndiyo watakaocheza nusu fainali ya kwanza. Nusu fainali ya pili itakuwa mshindi wa mechi ya Mara na Morogoro dhidi ya mshindi wa mechi ya Dodoma na Tanga.
 
Fainali itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu). Mechi zote kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA