Studio ya JK kukabidhiwa BASATA

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, amesema kuwa studio ya muziki iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii wa ndani bado haijazaa matunda na mpango wa kuikabidhi serikalini unafanyika.

Akizungumza bungeni mjini hapa juzi, alisema pamoja na nia njema ya kutaka kuwasaidia wasanii, lakini wajanja wachache wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa kutafuna fedha za studio hiyo.

Naibu waziri huyo aliongeza kuwa, wasimamizi hao wa studio wamethubutu kutafuna sh milioni 9.6 zilizotolewa na Rais Kikwete kwa ajili ya pango la studio hiyo na bila aibu wamekuwa wakiomba fedha nyingine kwa ajili hiyo.

Hata hivyo, Makalla alisema kuwa kutokana na studio hiyo kutokuwa na tija, serikali kwa sasa inafanya utaratibu wa kuirudisha serikalini na iwe chini ya usimamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Aidha, alitangaza kiama kwa baadhi ya wajanja, ambao wanafanya ujanja wa kuiba kazi za wasanii kwa kudurufu kazi zao kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe badala ya wasanii husika.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni bora wale wote wenye mitambo ya kudurufu kazi za wasanii, ambao wana tabia ya kuwaibia, wazirejeshe wenyewe la sivyo watachukuliwa hatua kali.

Akiendelea kuelezea hoja za kambi rasmi ya upinzani bungeni, Makalla alisema kuwa juhudi za Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr. II au Sugu, (CHADEMA), ambaye pia ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo, alisema ni msaada mkubwa kwa serikali na wasanii kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.