Sunday, July 1, 2012

Dkt Harisson Mwakyembe:Serikali kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

SERIKALI imesema kuwa ipo kwenye mchakato wa kuviboresha viwanja

mbalimbali vya ndege hapa nchini ukiwemo uwanja wa ndege wa Arusha kwa
kuufanyia matengenezo makubwa uweze kuruhusu kutua kwa ndege kubwa za
kimataifa.

Waziri wa uchukuzi ,Dkt Harisson Mwakyembe aliyesema hayo jana baada

ya kupokea taarifa fupi wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanja cha
ndege cha Arusha baada ya kufanya ziara fupi mkoani hapa.

Dkt Mwakyembe alisema kuwa uwanja wa ndege wa Arusha unaumuhimu wa

kipekee katika kuendeleza utalii wa ndani na kueleza kuwa serikali
itafanya kila njia kuhakikisha kuwa uwanja huo unapanuliwa na kuwa na
uwezo wa kutua ndege kubwa.

Alisema amekuwa akipata malalamiko mengi kuwa uwanja huo umekuwa

ukitumika kunyangánya wateja wa uwanja wa kimataifa wa
Kilimanjaro(KIA) huku maombi hayo yakitaka uwanja huo ufungwe.

‘’nimepata taarifa za kutaka kufungwa kwa  uwanja huu wa ndege wa

Arusha kwa kuwa unatumika kunyangánya abilia wa uwanja wa KIA
,nimejiridhisha kuwa kiwanja hiki kina umuhumu wa kipekee na serikali
itaangalia uwezekano wa kukiboresha’’alisema Mwakyembe.

Alisema serikali itatenga fedha zaidi  kwa ajili ya kukiboresha

kiwanja hicho ili kiwe cha kisasa zaidi ,ikiwa ni pamoja na
kuviboresha viwanja vingine vya Songwe,Kigoma na Mwanza.

Awali Kaimu mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha Arusha,Mhandisi

Suleiman Suleiman alisema kuwa kiwanja hicho kinakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa eneo la maegesho ya ndege, jengo
la abilia na jengo  la zima moto.

Alisema changamoto zingine ni pamoja na kutokuwa na taa zinazowaka

majira ya usiku hivyo kutoruhusu ndege kutua ama kuruka nyakati za
usiku,kituo cha umeme ,Mnara wa kuongozea ndege ,Jengo la hali ya hewa
,jengo la Mizigo  pamoja na miundombinu yake.

Aidha alisema kuwa ukarabati wa kiwango cha lami wa barabara ya kuruka

na kutua yenye urefu wa mita 420 uliogharimu kiasi cha shilingi
bilioni  1.7umefanya urefu wa barabara hiyo kufikia mita 1620 hivyo
kuwezesha  ndege zenye ukubwa wa kubeba abilia 70 kuweza kutua katika
kiwanja hicho.

Mhandisi Sulemeni aliongeza  kuwa kwa sasa kiwanja hicho kinahudumia

wastani ndege 1700 kwa mwaka na abilia wanaohudumia kwa mwezi ni
12,000.

Alisema kuwa mpango wa sasa ni kuhamisha barabara ya Arusha Babati na

tayari wamemweleza wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads).

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano uliopo sasa,

pamoja na kuhamisha barabara ya sasa ya kuingia kiwanjani hapo kwani
inaingiliana na maegesho. Chanzo; Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*