Tamasha la Wachagga Leaders leo

LILE tamasha la utamaduni wa Wachagga ‘Chagga Cultural Festival 2012’, linatarajiwa kurindima kwenye viwanja vya Leaders Club leo huku likisindikizwa na burudani kutoka kwa bendi mahiri za muziki wa dansi, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na bendi ya asili ya Mfalme chini ya Costa Siboka.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga, alisema kuwa, taratibu zote zilishakamilika na leo tamasha hilo litaanza kuanzia asubuhi mpaka usiku, ambako wadau mbalimbali watapata burudani na kujifunza tamaduni za kabila la Wachagga na mengine.

“Jumamosi hii ni siku ya pekee kwa familia, kujifunza mambo ya utamaduni wa Kichagga na makabila mengine huku wakisindikizwa na burudani kutoka kwa bendi za Twanga, Msondo na Mfalme chini ya Costa Siboka,” alisema Maganga.

Alisema kuwa, watakaobahatika kuhudhuria tamasha hilo, watakonga nyoyo zao na mbali ya kujifunza utamaduni wa kabila la Wachagga, pia watapata burudani kutoka bendi hizo ambazo zitapiga nyimbo zao mpya na za zamani, ambako pia warembo wa Miss Utalii Kinondoni watatembelea ili kujifunza utamaduni huo.

Alisema kuwa, katika tamasha hilo, kiingilio cha chini kimepangwa kuwa sh 5,000 huku cha juu kikiwa ni 25,000 pamoja na ‘bufee’ iliyo na vyakula vya kila aina ya kabila hilo.

Maganga alisema, wazee wa Mila wa Kichagga, watatoa elimu juu ya kabila hilo, watu watajifunza sambamba na kujua asili kwa undani ya Wachagga, ikiwemo vyakula na vinywaji vya asili kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.

Alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, na vingine vingi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA