Thursday, July 12, 2012

RAGE APASULIWA MGONGO INDIA


Rage kushoto; Hapa ni wakati anakabidhiwa madaraka na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu kabla yake, Mzee Hassan Daalal. BIN ZUBEIRY inamtakia kila la heri kiungo huyu wa zamani wa Simba na Tabora ''Mashujaa wa Unyanyembe, apone na kurejea kuendelea na shughuli zake za kila siku, zikiwemo za ujenzi wa taifa. Inshaallah. 

Na Princess Asia
MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye pia ni Mbunge wa Tabora (CCM), jana amefanyiwa upasuaji wa mgongo jana katika hospitali ya APOLO, India.
Daktari wa Simba SC, Cossmas Kapinga ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, sababu ya Rage kufanyiwa upasuaji huo ni maradhi yanayojulikana kitaalamu kama Lumbar Disc Prolapse.
Dk Kapinga alisema Rage, ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha Radio cha Voice Of Tabora (VOT) yuko kwa muda wiki moja nchini India akipatiwa matibabu na baada ya upasuaji huo wa jana, anaweza kupewa ruhusa kuanzia kesho kurejea nchini.
Kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Rage alikuwa kiungo wa klabu hiyo miaka ya 1970 na miaka ya 1980 aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu, wakati pia amekuwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (enzi za FAT), Makamu wa Pili wa rais wa TFFna Mjumbe wa Kamati mbalimbali za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).. (Chanzo; Bin Zubeiry Blog)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.