Mwananchi wa Kijiji cha Muyuni Shukuru Ramadhani akitoa maoni yake kuhusu katiba mpya huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mwenyekiti wa Ukusanyaji maoni ya Katiba Mpya Mohd Yussuf Mshamba akifahamisha namna ya utoaji wa maoni unavyotakiwa huko katika kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
 Wajumbe wa kukusanya maoni ya Katiba mpya wakiandika maoni ya wananchi huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mwananchi wa Kijiji cha Muyuni Mwanapili Haji Mussa akipeleka maoni yake kwa njia ya Barua yanayohusu uundwaji wa katiba Mpya kwa wajumbe wa Ukusanyaji maoni hayo huko Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
 Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika utoaji wa Maoni huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika utoaji wa Maoni huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
--
TUME ya taifa ya kukusanya maoni juu ya marekebisho ya Katiba inaendelea kukusanya maoni katika mkoa wa Kusini Unguja kwa wananchi mbalimbali ambapo inapokea maoni mbalimbali pamoja na kero za wananchi.

Wakitoa maoni yao kwa Tume hiyo wananchi wa Muyuni huko skuli ya Muyuni B wananchi hao wamesema wanataka kuwepo kwa mfumo utaweza kuondoa kezo zilizomo katika muungano ambazo ni changamoto kubwa  kwa wazanzibar. 

Aidha walisema wanataka kuwepo na serikali ya Zanzibar ambayo itakuwa na rais wake ambae anatambulika kitaifa na kimataifa , kuwepo na serikali ya Tanganyika na rais wake pamoja na serikali ya muungano ambayo itakuwa ya mkataba 

Wananchi hao waliitaka tume hiyo kuwepo na usawa katika serikali zote mbili zikiwemo mafuta, madaraka pamoja na utawala.

“Tunataka usawa na haki katika serikali zote mbili ambapo sisi wanzanzibar hatupati kitu katika muungano tunaomba marekebisho katika mafuta, madaraka na utawala”, walieleza wananchi hao.

Aidha baadhi ya wananchi hao wameitaka kuwepo na mfumo tofauti wa kielimu, kisarafu, kiulinzi pamoja na vyanzo vya mapato ili Zanzibar iweze kujitegemea wenyewe kimapato na kimaendeleo.

Hata hivyo wananchi hao waliiambia tume hiyo wanataka Zanzíbar iwe na mamlaka yake kamili na isiingiliwe katika maamuzi yake inayojipangia kama zilivyo nchi nyengine.

“Zanzibar haijapata mamlaka yake kamili tunataka tuwe na mamlaka ambapo tunataka isiingiliwe katika maamuzi yake wanachoamua wazanzibar kiwe hicho hicho kisibadilishwe”, walifafanua wananchi hao.

Baadhi wa wananchi hao walitaka kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu ambapo kutaweza kuwepo kwa usawa na mamlaka ya nchi pamoja na utawala wake na wengine walitaka kuwepo na marekebisho ya katika pamoja na kero za muungano.  
 
Na
Miza Kona 
Maelezo Zanzibar

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*