'USAJILI WA SIMBA MBOVU'

KOCHA wa timu ya Ports ya Djibouti, Issa Mvuyekure amesema Simba imesajili viungo wengi kuliko washambuliaji kitu ambacho kitawagharimu, huku akitupia lawama baadhi ya viongozi wa soka Tanzania kufanya kazi ya kocha hususani kwenye suala la usajili.

Alisema kwa jinsi alivyoiona Simba hakuna mshambuliaji aliyesukwa kwa ajili ya kazi hiyo zaidi ya kulazimisha kitu ambacho kwenye mechi za kimataifa na mashindano makubwa kama haya ya Kagame yanayoendelea ni hatari.

"Naifahamu Simba tangu nikiwa mwalimu wa Kahama United na mara nyingi nabahatika kuiona kwenye mechi za kimataifa, lakini wanachokifanya katika mashindano ya Kagame siyo nilichokizoea, hii inatokana na kukosa washambuliaji,"alisema Mvuyekure.

Alisema,"licha ya kunifunga mabao 3-0 sikutegemea, nilijua nitafungwa mabao mengi sana, Simba ikitaka kusonga mbele iongeze washambuliaji badala ya kujaza viungo kwani kuna timu zimejipanga vizuri, kama wamecheza na wachezaji wangu wala tambi na kupelekwa puta, siku wakicheza na timu ambazo wachezaji wake wana nguvu watafungwa mabao mengi."

Alisema kuwa kwa mpira wa Simba aliouona haamini kama walicheza na URA ya Uganda na kufungwa mabao 2-0 pekee.

"Simba itasonga kibahati, pia inatumia uwanja wa nyumbani, lakini kwa soka la Simba inayojulikana na nchi zote za Ukanda huu wa Afrika sio ile niliyoiona, kocha ana kazi ngumu na sijui kwa nini amefanya usajili wa aina ile,"alisema Mvuyekure.

Mvuyekure hakusita kupeleka lawama zake kwa baadhi ya viongozi wa timu akidai kuwa ni chanzo cha timu nyingi kufanya vibaya kwani kazi ya usajili ni kazi ya kocha, lakini wanafanya wao.

"Nilifanya kazi Tanzania, niliacha kutokana na kupangiwa cha kufanya na uongozi haswa suala la usajili badala ya usajili kufanya kocha kutokana na mahitaji ya kikosi chake,"alisema Mvuyekure ambaye ni raia wa Burundi anayefundisha soka Djibouti.

Alisema,"hapa Tanzania usajili wa wachezaji wanafanya viongozi na hawaangalii kiwango ila maslahi yao iwe ya kindugu au kirafiki na kama tabia hiyo ipo kwenye timu ya Simba itamsumbua sana kocha, mimi nilishindwa na nikaamua kuacha kazi nikarudi Burundi kuanza upya."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI