USITUMIE FEDHA, ELIMU KUMNYANYASA MWEZA WAKO

KUWA na fedha au elimu zaidi ya mwenzi wako, sio tiketi ya kumfanya asiwe na raha kama ambavyo wamekuwa wakifanya baadhi ya watu.

Wala kutokuwa na fedha au elimu ama umaarufu haina maana kwamba uwe ni mtu wa kunyanyaswa.Ukweli ni kwamba unapokuwa kwenye uhusiano, kilicho cha msingi ni kwa kila mtu kufanya awezalo kupeana raha.

Kama unafikiri uko na mwanamke wako ili umnyanyase kwa sababu labda una fedha zaidi au umaarufu zaidi yake, hilo ni kosa na fahamu kuwa unasababisha maisha yako katika suala la ndoa kuwa mabaya.

Hata kama labda mwanamke ana fedha zaidi ya mumewe, au ana umaarufu zaidi ya mumewe, si vema kutesana katika mapenzi. Unapoamua kumpenda fulani, ni vizuri ukamaanisha hilo kwa vitendo.

Kama utasema nampenda fulani halafu unamtesa, maana yake ni kwamba unamfanya huyo akuchukie; aidha anaweza kuendelea kubaki na wewe akiwa anaumia, lakini zaidi, wengine huamua kuanzisha uhusiano na wengine.

Matokeo ya mwenza wako kuanzisha uhusiano na mwingine, maana yake katika lugha rahisi ni kwamba anakuwa ana uwinda uliko Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.

Unaweza kumtesa mwenza wako, lakini fahamu kwamba yeye ni mwanadamu, unaweza kumpiga mangumi,yeye atakupiga kwa kukuambukiza Ukimwi. 

Mwenye hekima anapswa kutafakari kwa umakini mkubwa unapomtesa au kumnyima raha mwenza wako.

Unaweza kujifanya mjanja, lakini ujanja wako ni sawa na upumbavu...unamtesa mkeo au unamtesa mumeo, anaishi kwa shida, kisha unamwambia naomba tendo la ndoa...Teh! Teh! Teh! Tayari umekuwa ni kero kwake, anakupa basi afanyeje, lakini labda kishafanya na wengine na sasa ana Ukimwi anakupatia!

NI HEKIMA KUIFANYA NDOA YAKO IWE NA AMANI
Katika maisha ni vizuri kuwa makini sana na mambo ambayo unamfanyia mwenzi wako. Kuna wengi kwa mfano wako kwenye ndoa, hawana uhakika wa kupata tendo la ndoa...hilo ni kosa. Je, wewe katika ndoa yako hali ikoje? 

Pata muda wa kufakari matendo yako kwa mwenzi wako. Kwa vyovyote inavyokuwa, unapaswa kuangalia namna ya kufanya ili mwenzi wako aweze kuwa na amani ya kweli kama mwanandoa.

USITUMIE FEDHA KAMA FIMBO, MPAKA PALE PATAKAPOKUWA NA MAKUBALIANO HAPO FEDHA NDIO HUWA INA THAMANI

Ni kwamba fedha inatumika kununuliana zawadi, kufanya mambo ya maendeleo katika familia na mambo mengine yanayofanana na hayo. Kinyume na hilo sio sahihi kuitumia fedha kwa ajili ya kutesana au kuonyeshana ufahari au majivuno kama wanavyofanya baadhi ya watu.

Kuna wanaume wengine wana magari, wenye kuyapanda ni nyumba ndogo...mkewe hata aumwe anaambiwa aaah chukua taksi fedha hiyo hapo...hii si sawa. Watu hawajaingia kwenye ndoa kutafuta fedha, bali kusaka upendo thabiti.

UVUMILIVU NI MUHIMU 
Mara nyingi sana nimekuwa nikisema ndoa yahitaji uvumilivu lakini sidhani kama naeleweka ipasavyo juu ya hili neno. Ukweli ni kwamba ndoa, kama yalivyo maisha ya aina nyingine yanatuhitaji kuvumiliana.

Kwenye mapenzi ya dhati uvumilivu hutangulia, na hii hutokana na ukweli kwamba upendo huvumilia. Panapo upendo ule usiosukumwa na mambo ya nje bali ule wenye msukumo wa ndani tu uvumilivu hutangulia na hii ni kwasababu kuu mbili nazo ni uvumilivu huona mapungufu ya mwenza wako kama changamoto wala si kama chuki.

Uvumilivu hauhesabu gharama za kazi, upendo ,kujitolea ama hela. Kama kweli unapenda kwa dhati, hakika utavumilia.

Iwe ndoa, urafiki,familia, hata kufanya kazi pamoja uvumilivu una nafasi kubwa sana. Ndio maana hata baadhi ya familia wakigombana AMA kutofautiana ni matusi ambayo hata kwenye kamusi hayamo.

Wengine kila kitu ni kusutana na kupaza sauti. Hata ndoa pia Kama ilivyo kwenye kazi na familia kunahitajika kiwango fulani cha uvumilivu.

 Ila kuna mambo yasiyohitaji kuvumilia kutoka nje ya ndoa na kutesana mwili kwa waziwazi.



Ambacho nataka ubaki nacho kupitia makala hii ya leo ni kwamba usitumie fedha, elimu kumtesa mwenza wako, bali mlikubaliana kuwa wapenzi, tendeaneni yaliyo ya amani.
Kwa ushauri zaidi 0653777700 au 0755444555

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.