WABUNGE KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII WAPATA SOMO BIMA YA AFYA

 Ofisa Nyaraka wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Erastus Msigwa akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, jinsi wanavyohifadhi kwa njia ya kisasa kadi za wananchama wa mfuko huo, wakati wa wa semina waliyoandaliwa wabunge leo katika Makao Makuu ya NHIF, Dar es Salaam.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Ofisa Nyaraka wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Erastus Msigwa akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, moja ya mafaili ya wananchama yanayohifadhiwa kwa njia ya kisasa kadi za wananchama wa mfuko huo, wakati wa wa semina waliyoandaliwa wabunge leo katika Makao Makuu ya NHIF, Dar es Salaam.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Meneja Idara ya Uanachama wa NHIF, Ellentruder Mbogoro, akitoa maelezo kwa wabunge jinsi wanavyohifadhi mafaili ya wana chama kwa njia ya kisasa
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akifafanua jambo wakati wa semina hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba (kushoto) akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Seif , ambao pia walihudhuria semina hiyo.

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Emmanuel Humba ametoa ombi maalumu kwa Serikali kuunda chombo kitakachodhibiti mfumuko wa gharama za matibabu.

Humba alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati akizingumza na  wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya huduma za jamii ambao wamefika makao makuu ya mfuko huo kwa ajili ya kuona shughuli mbalimbali za mfuko lakini pia kutumia nafasi hiyo kupata ufafanuzi wa mambo muhimu ambayo wanahitaji kuyafahamu.

Akifafanua zaidi mbele ya wajumbe hao, Humba alisema pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili bado ombo lao kubwa kwa Serikali kuunda chombo hicho kitakachosaidia kudhibiti gharama za matibabu.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwaomba wajumbe wa kamati hiyo ambao ni wawakilishi wa wananchi, kusaidia kuhimiza usimamizi na udhibiti wa fedha zinazochangwa na wananchi katika Mfuko wa Afya ya Jamii na zile wanazolipa kwenye halmashauri  ili ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa kama ununuzi wa dawa.

"Waheshimiwa wabunge , kupitia fursa mlizonazo kwa wananchi, tusaidieni kuwahamasisha wananchi kujiunga na mifuko hii kwa kuwa ndio mkombozi na yenye uhakika wa kupata matibabu kwa wakati wowote,"alisema.

Kuhusu changamoto ,Humba alisema mfuko bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea  huduma ambayo inakwamisha jitihada na nia njema ya Serikali  katika kufikia lengo  la kuwa na wigo mpana wa wananchi walio kwenye utaratibu wa bima ya afya.

Pia kukosekana chombo kinachodhibiti bei za dawa na huduma za afya hususani vijijini hali inaypsababisha malalamiko kutoka kwa wanachama wao, hasa wanapochelewa kupata huduma kwa wakati.

Akizungumzia mfuko huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi pamoja na changamoto zilizipo bado umeweza kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma za afya kwa wananchi na hasa wanachama ambao wamejiunga na kwamba Serikali itaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga zaidi ya mifuko ya afya.

Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, walisema kuwa kimsingi wameridhishwa na mfuko wa utunzaji wa kumbukumbuku za wanachama wa mfuko huo lakini bado wanaona iko haja ya kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi ili waweze kujiunga na hatimaye kupata huduma za afya.

Hata hivyo walisema bado kuna malalamiko kwa baadhi ya wanachama wa mfuko huo ambao wamekuwa wakipata huduma za kiwango cha chini wanapokwenda kwenye vituo vya afya wakati wanakatwa kwa ajili ya huduma hizo jambo ambalo sasa linahitaji kuangaliwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA