Wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wakamatwa

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

. ZAIDI ya wafuasi  40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibr wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana  kwenye eneo la Darajani mjini Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa mawe, vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.
Kamanda Aziz amesema kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa kikundi hicho waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo zilizokuwa nimeendelea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar.
Amesema wafuasi hao walitumia mawe, chupa  na vipande vya mbao kuwarushia Polisi lakini amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa nane usiku wa kuamkia leo,
Hata hivyo Kamanda Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi wa kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.
Amesema vurugu hizo ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu hadi saa 8.00 usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika maeneo mbalimbali wakifanya vurugu.
“Tunawatafuta viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na kujisalimisha wenyewe Polisi.” Alisema Kamanda Aziz.
Mara baada ya kuanza kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za Darajani na mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, ilikuwa haia hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama.
Hata hivyo biashara mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku watumishi wa Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji wa mawe, matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.
Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma za kuanzisha gha

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA