Wahamiaji haramu wajiandikisha vitambulisho vya taifa

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya wahamiaji haramu wamejiandikisha na kujaza fomu za maombi ya vitambulisho vya uraia.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kwenye kituo kimoja Mtaa wa Ali Hassan Mwinyi, eneo la Mikocheni A, wakiwa wamejitokeza kujaza fomu hizo bila vithibitisho halali vinavyowaruhusu kuishi nchini.

Hata hivyo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) ilisema wahamiaji wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini, hati ya kusafiria au cheti cha ukimbizi hawatatambulika na kuhusishwa katika zoezi hilo na kubainisha kuwa, kwa wageni kuishi nchini bila vitu hivyo ni kinyume cha sheria.

Ofisa Habari wa Nida, Thomas William alisema iwapo itabainika kuna wahamiaji haramu wamefanikiwa kujiandikisha katika hatua za awali, mamlaka hiyo itashirikiana na Idara ya Uhamiaji kuwawajibisha.
“Kama kuna wahamiaji haramu ambao hawana vibali wala hati za kusafiria, lazima tutawabaini na kuhakikisha tunawafikisha ngazi husika kwani mchakato bado ni mrefu tutawapata tu,” alisema William.

Aliongeza kuwa Mamlaka hiyo imeweka kamati ya ulinzi na Usalama katika kila kata ili kuahkikisha hakuna udanganyifu utakaofanyika kwa lengo la kupotosha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine William alisisitiza kuwa zoezi hilo litawahusisha watanzania walio nje ya nchi ingawa alibaionisha kuwa Mamlaka haijatoa muda rasmi wa wao kurudi nchini ili kujisajili.

“Hata wale walioko nje ya nchi wanapaswa kurudi kujiandikisha na kupata vitambulisho hivi, lakini ingawa mamlaka haijasema warudi sasa kwa kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ila kujiandikisha ni lazima kwa Watanzania wote,” alisema William.

Pia, aliwatahadharisha Watanzania kutotoa fedha kuandikishwa au kujaza fomu hizo, kwani zoezi hilo linaratibiwa na Serikali.

“Zoezi hili halipaswi kulipiwa na mamlaka imepata taarifa za baadhi wa watendaji wa Serikali kudai fedha kwa ajili ya kuandika barua za utambulisho kwa wakazi wa maeneo yao,” alisema
Alitaja maeneo ambayo watendaji wake wamekamatwa kwa tuhuma hizo kuwa, ni Bunju, Mabwepande na Yombo Vituka.

Aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika vituo wakiwa na vitambulisho vyao kushiriki zoezi hilo ambalo litakamilika rasmi Julai 30, mwaka huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.