WANAKIJIJI WANYANG'ANYWA MRADI WA KIWANDA ILUNDO KIWIRA




WAKAZI wa kijiji cha Ilundo kata ya Kiwira wilayani Rungwe sasa
watajilaumu kwa kuukosa mradi mkubwa wa kiwanda cha matunda kufuatia
vurugu walizozifanya mapema mwezi Mei mwaka huu

Kiwanda hicho ambacho ujenzi wake utagharimu shilingi 45,996,000 ikiwa
ni fedha kutoka Mpango wa Maendeleo ya kilimo(DADP’s) sasa kitajengwa
katika kijiji cha Iponjola kata ya Lufingo.

Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kupitia kikao chake lilipitisha
maamuzi ya kuhamishwa kwa mradi huo huku likisisitiza kuwa hali hiyo
huenda ikayakumba maeneo yote yanayoonekana kukithiri kwa migogoro.


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Meckson Mwakipunga alisema Vurugu za
kijiji cha Ilundo zilisababisha wadau kukosa imani ya eneo hilo kuwa
na Amani na Utulivu kiasi cha kupeleka mradi unaogharimu fedha nyingi.

Mwakipunga alisema miongoni mwa matukio yaliyowakatisha tama ya
kuwekeza katika kijiji hicho ni wanakijiji hao kuvunja jingo la
zahanati iliyokuwa mbioni kufunguliwa pamoja na ofisi ya serikali ya
kijiji cha kwa madai ya kutomtaka mwenyekiti wao.

“Kufuatia uharibifu wa mali za umma uliofanyika,kamati yangu ya
Fedha,Utawala na Mipango baada ya kuliangalia suala hilo kwa kina na
kutoridhika na mwenendo wa hali ya usalama unaoendelea mpaka sasa
kijijini hapo”

“Iliazimia mradi wa ujenzi wa kiwanda cha matundauliopangwa kuanza
utekelezaji 2011/2012 lakini ulikuwa bado usitishwe na badala yake
kiwanda hicho kujengwa sehemu nyingine nje ya kijiji hicho” alisema.

Alitaja sifa za kijiji kulikohamishiwa mradi huo kuwa ni pamoja na
huduma ya maji ya kutosha,miundombini ya barabara ya uhakika kwa mwaka
mzima,umeme kwaajili ya kuendesha mitambo.

Sifa nyingine ni kufikika kwa urahisi na maeneo mengine kunakozalishwa
matunda na pia uwezekano wa upatikanaji wa eneo la kutosha kwaajili ya
ujenzi wa miundombinu muhimu ikiwemo majengo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.