WATEJA LUKUKI WANUFAIKA NA ZAWADI ZA DROO JENGA MAISHA YAKO NA NMB

 Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB, Josephine Kulwa, akibofya kwenye kompyuta kupata washindi wa promosheni ya  "Jenga Maisha yako na NMB" katika hafla iliyofanyika, Dar es Salaam leo. Washindi ambao  ni wateja wa benki hiyo, watazawadiwa  saruji, mabati, fulana, mabegi, ada ya shule na kuongezewa  amana maradufu. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Bidhaa  wa Kampuni ya Selcom Wireless, Julio Batalia (kulia) na  Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha nchini, Sadiki Elimsu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA),

                                                  Kulwa akizungumza katika mkutano huo
                                                       Wanahabari wakiwa kazini

                              Camera woman Faraja Kihongole wa Chanel Tv akiwa kazini

NMB kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea yakiwa  ni kujenga nyumba,kusomesha watoto na  kufikia malengo mengine  muhimu maishani mwao,  ilizindua promosheni inayowezesha wateja wa NMB Bonus Account an NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda tani ya saruji,mabati ya kuwezeka,amana maradufu,ada za shule,fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule kupitia promosheni ya Jenga maisha yako na NMB.
Hivyo basi, leo droo ya Jenga maisha yako na NMB imechezeshwa na washindi zaidi ya 167 wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tani za seruji na mabati ya kuwezekea.
Katika picha juu ni Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia na Mkuguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mawasiliani wa NMB,Josephine Kulwa alisema “NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliojiwekea na pia kuboresha maisha yao”
 
Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.
Zawadi zilizoshindaniwa kwenye droo ya leo
Zawadi
Namba ya washindi
Tani ya saruji (simenti)
8
Mabati
3
Double your account
3
Mabegi ya shule
100
Ada zashule
3
Tisheti za NMB
150
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.