Yanga yakubali 2-0 kwa Atletico ya Burundi

Kikosi cha timu ya Yanga ya Tanzania kabla ya mpambano wake na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kombe la Kagame la Klabu bingwa ya Afrika ya Mashariki na Kati, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Kikosi cha timu ya Atletico ya Burundi kabla ya mpambano wake na Yanga ya Tanzania katika mchezo wa Kombe hilo, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni.

Mchezaji Haruna Niyozima wa Yanga (kushoto), akichuana na Gael Duhayindavyi wa Atletico ya Burundi wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame la Klabu bingwa ya Afrika ya Mashariki na Kati, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, ilikubali kipigo cha mabao 2-0, dhidi timu hiyo.

Hamis Kiiza wa Yanga, akiruka juu kukwepa kwanja la mchezaji Francis Nongwe wa Atletico ya Burundi wakati wa mcezo huo leo.

Haruna Niyozima wa Yanga (kulia), akijaribu kumtoka Gael Duhayindavyi wa Atletico ya Burundi wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame la Klabu bingwa ya Afrika ya Mashariki na Kati, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Yanga ilikubali mabao 2-0, dhidi timu hiyo.

Haruna Niyozima wa Yanga (kulia), akipambana na Gael Duhayindavyi wa Atletico ya Burundi katika mchezo huo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni.

Mashabiki wa timu ya Yanga, wakifuatilia mchezo huo, wakati timu yao hiyo, ilipokuwa ikipambana na Atletico ya Burundi.

Mchezaji Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi akifunga goli la kwanza la timu yake dhidi ya Yanga. Anayemkimbilia kumkabili ni Athuman Idd 'Chuji'.

Mchezaji Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi akifurahia bao lake hilo, mara baada ya kumvuta golikipa Yaw Berko wa Yanga (hayupo pichani) na kumtungua kushotoni kwa golini kwake.

Mashabiki wa timu ya Simba, wakiwashangilia Atletico ya Burundi mara baada ya kushinda goli hilo la kwanza katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.

Mchezaji Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Ladislaus Mbogo wa Yanga.

Mchezaji Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi akikimbia kufurahia goli lake la pili baada ya kumtungua golikipa Yaw Berko (kulia aliyepiga goti) wa Yanga katika mchezo huo.

Mchezaji Ladislaus Mbogo wa Yanga, akiutoa mpira wavuni baada ya Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi, kufunga goli la pili kwa timu yake hiyo.

Didier Kavumbangu wa Atletico ya Burundi, (katikati), akifurahia kwa kucheza pamoja na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli hilo kwa timu yake hiyo na kuipatia pointi 3.

Hadi mchezo huo unamalizika ubao wa matokeo ulikuwa ukionesha Yanga (Tz) 0 Atletico (Bur) 2.

Wachezaji wa timu ya Atletico ya Burundi wakiwapungia mashabiki wa Simba waliokuwa wakiwashangilia katika mchezo huo baada ya mchezo huo kumalizika wakiwa washindi. Chanzo Bayana Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU