AJINYONGA AKIDHANI AMEUA MKE BAADA YA KUMSHAMBULIA KWA PANGA


 Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma,  Zelothe Stephen. 
******************************
Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamuhuri John, mwenye umri wa miaka (28)amekutwa amejinyonga katika mti wa mbuyu baada ya kuwajeruhi kwa Panga mke na mtoto wake kisha kukimbia kusikojulikana.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Edmundi Urio  alisema tukio hilo la kujinyonga liligundulika mnamo tarehe 17/08/2012 majira ya saa 06:45 asubuhi, na wananchi waliokuwa wakimfuatilia katika Kijiji cha Kikombo Kata na tarafa ya Kikombo Wilaya ya Dodoma Mjini.

 “Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mtu huyo ni ugomvi wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amewajeruhi mke na mtoto wake kwa kuwakata na mapanga kisha kukimbia kusikojulikana hadi alipogundulika amejinyonga.“ Alielezea Kamanda Edmundi Urio.
Bw. Urio alieleza kwamba Marehemu alikuwa na ugomvi na mke wake kwa muda mrefu kitu kilichopelekea mwanamke huyo kutoroka nyumbani kwake na kukimbilia kwenda kuishi Tanga inakodaiwa kuwa ni kwa baba yake mzazi.

Kamanda Edmund Urio alisema, baaada ya kukaa muda mrefu bila kumuona mke wake marehemu alikuwa na wasiwasi kuwa ameolewa, hivyo aliamua kumtafuta mke wake huyo na ndipo alipoamua kwenda kwa mtendaji wa Kijiji hicho cha Kikombo Bw. Wenos Dede kuomba barua ya kumtafuta mke wake Tanga na kupatiwa barua hiyo.

Aidh Bw. Urio alieleza kwamba Jana majira ya saa mbili usiku marehemu na mke wake wakiwa wanarudi toka Tanga walipewa maelekezo kwamba, wafike kwanza kwa mtendaji kumjulisha na kwa usuluhishi zaidi, walipofika   hawakumkuta mtendaji kwa kuwa alikuwa amekwenda kuhudhuria  semina ya mambo ya Sensa katika Kijiji cha Ihumwa.

“Hivyo wakiwa njiani walishindwa kuelewana, kwani mwanamke alikuwa anataka kwenda kulala kwa bibi yake hapo hapo kijijini, ili kesho yake wamtafute mtendaji ili wamalizane lakini mume wake alikataa na kumwambia amsubiri akachukue shuka ndipo akakimbia nyumbani kwao akachukua Hengo na kulificha katika koti kisha kurudi na kuanza kumshambulia mke wake.” alieleza Kamanda Urio.

Kaimu Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma, alimtaja mwanamke huyo aliyejeruhiwa kuwa nia Aksa John, mwenye umri wa miaka (21), mgogo na mkazi wa Kikombo, pamoja na mtoto wake aitwaye Gerald John mwenye umri wa miaka (4) aliyejeruhiwa kwa kukatwa Panga katika mguu wake wa kushoto. 

Alisema mwanamke huyo amejeruhiwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia chini ya kiganja, na mkono wa kushoto kidole chake gumba kilikatwa kabisa pamoja na kujeruhiwa katika mguu wa kushoto karibu na sehemu ya kukanyagia.

Kamanda Urio Amesema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, ambapo Mama huyo amelazwa katika wodi namba nane wakati mtoto wake amelazwa wodi namba moja na kwamba wanaendelea vizuri. 

Imetolewa na
Jeshi la POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone:  0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone:  0712  360203, Silyvester Onesmo – Police  Konstebo  (PC)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.