AUDITION YA 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' YAVUTA WASHIRIKI ZAIDI YA 100 JIJINI DAR

Casting Coordinator wa ALLY REHMTULLA'S COLLECTION 2012 Audition Martin Kadinda akitoa mwongozo wa zoezi hilo kwa Models walioshiriki.
Baadhi ya Models wa kiume waliojitokeza Serena Hotel wakisubiri usaili.
Pichani Juu na Chini ni Models wa kike na wa kiume wakipita mbele ya Majaji wakati wa usaili.
Meza kuu ya Majaji kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Alliance Auto Bw. Alfred Minja akiwakilisha CFAO Motors wauzaji wa Magari ya Mercedes Benz ambao ndio wadhamini wakuu wa 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013', Aysha Mbarak Meghji kutoka Ayman Garage-Convolution Ideas Ltd, Administrative Assistant Mawalla Advocate na pia ni Model Myler Nyangasa, Mwasisi na CEO wa Missie Popular Blog Mariam Ndabagenga na Fashion Stylist wa Fashionnjukii.com Rosemary Kokuhilwa.
Pichani Juu na Chini Models wa kike wakionyesha umahiri wa Catwalk wakati wa Audition kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki "ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013".
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Models wa kiume wakipita jukwaani mbele ya majaji.
Baadhi ya Models wakiwa katika tafakari ya SIJUI NITAPITA wakati wa usaili huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed ambao ni wauzaji wa magari aina ya Mercedes waliodhamini onyesho la 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' akielezea kuwa Mercedes Benz imedhamini Onyesho hilo kwa mara ya kwanza kwa sababu kwanza wanamkubali Ally Rehmtullah kama mmoja wa wabunifu wenye hadhi ya juu hapa nchini na kuwa wamechagua Brand ya Mercedes Benz kwa sababu ni magari yenye kiwango cha juu na Rehmtullah ana ubunifu wa hali ya juu.
Mercedes Benz imekuwa ikijihusisha na udhamini wa 'High and Fashion Show' duniani kote pia Orchestra, Baley na Sailing matukio ambayo yanaendana na hadhi ya magari ya Mercedes. Kulia ni Chief Editor wa MO BLOG Lemmy Hipolite.
Sales & Marketing Representative kutoka RAHA Preetkamal Bansal akielezea kuwa kampuni yake imekuwa na furaha kushirikiana na Ally Rehmtullah kwa kuwa ubunifu wake ni wa hali ya juu kama wao wanavyotoa huduma za Intaneti za hali ya juu na wamekuwa wakitoa huduma ya ISP (Internet Service Provider) kwa muda wa miaka 16 kwa kiwango kilekile.
RAHA wakiwa wadhamini muhimu watawezesha watu kuona Live 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' itakayofanyika September 8 mwaka huu ambapo Watu duniani kote wataona kupitia http://www.ar.co.tz/.
Amemalizia kwa kusema "On the day the Jungle puts on its show Our Broadband let you watch it Live".
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quality Furniture Limited Bw. Mahad A Nur akisema wameamua kujihusisha kudhamini show hii ya Ally Rehmtullah ili kutoa ufahamu kwa umma juu ya ubora wa bidhaa wanazotengeneza na siku ya Onyesho hilo watatoa Furniture zitakazotumika sehemu ya wageni maalum (VIP).
Quality Furniture Limited wanatengeneza bidhaa zenye Quality kama lilivyojina lao na kama ilivyo show ya Ally Rehmtullah lakini pia Bw. Mahad amesema wako tayari kuwadhamini wabunifu chipukizi watakaokuja na ubunifu wenye Quality.
Majaji Aysha Mbarak Meghji na Rosemary Kokuhilwa wakibadilishana mawazo baada ya kazi kubwa ya kuchagua Models watakaoshiriki 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013'.
Ally Rehmtullah.
Hawa pia nao walikuwepo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*